Jeshi la polisi mkoani Dodoma linamshikilia Askofu, Martin Gwila wa kanisa la Agape Sanctuary International kwa tuhuma za utapeli wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 63.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto amesema kiasi hicho cha fedha alikipata baada ya kuwadanganya watu mbalimbali kuwa atawapa ajira kupitia kanisa lake.

Pia anadaiwa kuwalaghai waumini akiwataka watoe fedha ili wasajiliwe na kuwatoza waumini wake kiwango tofauti cha fedha.

”Askofu huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki jijini Dodoma na alipokea fedha hizo pasipo kutoa ajira yoyote huku akitoa vitisho kwa waliotoa fedha hizo” amesema Muroto.

Kamanda Muroto amesema kuwa kanisa hilo ambalo makao yake makuu yapo Arusha halijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kama kanisa bali limesajiliwa kama kampuni binafsi ya Agape sanctuary.

Aidha mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

JPM amteua Jaji Lubuva
CUF yaipongeza serikali kwa kukuza uchumi