Hali ya kiafya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi inaendelea kuimarika mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo na madaktari bingwa katika hospitali ya Muhimbili (Moi).

Na sasa amehamishiwa katika wodi ya kawaida kutoka katika chumba cha ICU alichokuwa amelazwa.

Kwa mujibu wa jopo la madaktari bingwa 7 wanaomuhudumia wamesema kuwa upasuaji wa Ubongo uliofanyika kwa kiasi kubwa umemsaidia hivyo wameamua kumhamisha chumba cha ICU.

Profesa Joseph Kahamba amesema baada ya kutolewa mashine iliyokuwa inamsadia kupumua askofu Ruwa’ichi amekuwa akiendelea vizuri na kufanya mazoezi.

Askofu Ruwa’ichi alifikishwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (Moi) akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo.

Mwanafunzi wa shule ya msingi akana kupewa mimba na mkuu wa shule
Mabao ya Molinga 'Falcao' kununuliwa kwa mamilioni