Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene ameondolewa katika idara hiyo na kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia kupitia kitengo cha Mawasiliano Serikalini imeeleza kuwa uhamisho wa Mwambene ni wa kawaida na kwamba atapangiwa kazi nyingine katika Wizara aliyohamishiwa.

Kutokana na hatua hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel amemteua Zamaradi Kawawa kuchukua nafasi aliyokuwa nayo Mwambene.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Zamaradi anashikilia kwa muda nafasi hiyo ikisubiri uteuzi rasmi, huku akiwa ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uratibu wa Mawasiliano Serikalini katika Wizara hiyo.

 

Coastal Union Kutangaza Msimamo Wa Kujinusru Kushuka Daraja
Picha: Magufuli atekeleza agizo la Makonda, awasilisha silaha yake