Klabu ya AC Milan imethibitisha taarifa za kukamilisha usajili wa kiungo kutoka nchini Argentina Lucas Biglia akitokea SS Lazio ya Italia kwa ada ambayo imefanywa kuwa siri.

Biglia mwenye umri wa miaka 31 aliwahi kutwaa ubingwa wa nchini Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht kabla ya kutimkia SS Lazio mwaka 2013. Msimu uliopita alifunga mabao manne katika michezo 29 alyocheza akiwa na klabu ya SS Lazio iliyomaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya nchini Italia.

“AC Milan inayo furaha kuwafahamisha mashabiki wake popote pale ulimwenguni, tumemsajili Lucas Biglia baada ya kumalizana na  SS Lazio. Mchezaji huyo amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu, na atakua hapa hadi Juni 30 mwaka 2020,” ni taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya klabu hiyo ya mjini Milan (www.acmilan.com).

“Biglia ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, na ana kipaji ambacho kitaisaidia AC Milan katika harakati za kusaka mafanikio msimu ujao, Kufanikisha kumsajili mchezaji huyu, inadhihirisha tunaendelea kutengeneza kikosi chenye wachezsaji imara. Hivyo Biglia ni mchezaji muhimu ambaye tulihitaji kumsajili tangu tulipoanza harakati za usajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.”

Video: Maimamu watoa neno kwa JPM kuhusu Masheikh wa Uamsho
Nolito Arudi Nyumbani Hispania