Klabu ya Aston Villa imetangaza kumuweka pembeni kwa muda mshambuliaji wake Gabriel Agbonlahor, baada ya kuibuka taarifa za kiponda raha, akiwa Dubai.

Aston villa wametangaza hatua hiyo, ili kupisha uchunguzi unaofanywa dhidi ya Agbonlahor, ambaye anadaiwa kuvunja taratibu za kimaadili za klabu hiyo kwa kuvuta Shisha hadharani.

Madhila hayo yanadaiwa kutokea wakati wa mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ya kirafiki, ambapo baadhi ya wachezaji wa Aston villa walipewa ruhusa ya kupumzika kwa siku kadhaa.

Agbonlahor ameripotiwa alikwenda Dubai sambamba na nahodha wa Aston Villa, Micah Richards na huko ndipo alipoponda raha hadi kufikia hatua ya kwenda kinyume na taratibu za kinidhamu.

Agbonlahor at his boozy birthday bash

Baadhi ya picha za mchezaji huyo zimevuja kwa kuonekana akivuta shisha hadharani na nyingine zikimuonyesha akiwa amepoteza fahamu na kuburuzwa na mtu ambaye hajajulikana kwa urahisi.

Kutokana na maamuzi ya kuweka pembeni Agbonlahor, hatokuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea ambao utakua na umuhimu mkubwa kwa The Villians ambao wanachungulia shimo la kushuka daraja.

Picha Ya Timu Ya Taifa Ya Ujerumani Yazua Tafrani
Twiga Stars Yaomba Kujikabidhisha Kwa Serikali