Msanii wa miondoko ya mduara na muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Ally Ramadhani maarufu ‘AT’, amesema kuwa yeye amemzuia mke wake kuingia jikoni kupika badala yake anapika mwenyewe.

AT amedai kuwa wanawake hawajaletwa duniani kuteseka bali kupendwa na kuhudumiwa hivyo licha ya kumpikia mkewe pia hutandika kitanda.

Amesema yeye kufanya hivyo ni sehemu yake ya utekelezaji wa majukumu yake kama inavyotakiwa wanaume kuwahudumia wake zao.

” Mke wangu ana roho ya kipekee sana, alishawahi kuwekewa sumu na akasamehe, mke wangu kwanza hapiki nilimzuia, mimi ndiye nampikia, namfulia  na kumtandikia kitanda, ubwege sikuzote unalinda mahusiano” amesema AT.

Aidha amesema wanawake wengi huteseka kwenye mahusiano kwa sababu wao wametokana na binadamu, ndiyo maana wana huruma ukilinganisha wanaume ambao wametokana na udongo ambao kwa asilimia kubwa hawana huruma.

Simba Vs Yanga: Wakubali sare ya piga-nikupige, fahamu nani alimzidia nani
DC Same atangaza kiama Polisi wenye urafiki na wahalifu, atoa siku 30 kusalimisha silaha

Comments

comments