Mkali wa Miduara, AT amesema kuwa chanzo cha ugomvi kati ya mafahari wawili wa muziki wa bongo fleva, Diamond na Ali Kiba ni penzi la muigizaji wa kike, Jacqueline Wolper.

Akifunguka kupitia Shilawadu ya Clouds TV, AT ambaye alieleza kuwa wawili hao walitaka kuzichapa ngumi kavukavu ndani ya chumba chake nchini Oman walikokuwa wameendea kufanya tamasha moja, alisema kuwa katika harakati za kutoleana maneno, Ali Kiba aliweka wazi kuwa mrembo ndiye chanzo cha yote.

Alisema kuwa Ali Kiba alimvaa Diamond kwa maneno baada ya kukwaruzana, akimueleza kuwa alikuwa akimtafuta siku nyingi kwani ameshasikia maneno yake akimponda kwa mrembo ambaye anasadikika kuwa ni Wolper, kuwa ameshapotea kimuziki hivyo mrembo huyo abaki naye.

“Wakati huo Ali Kiba alikuwa ameshaachana na Wolper, lakini ana uhusiano na Diamond. Kwahiyo Ali Kiba ingawa hakumtaja jina, alisema ‘mimi yule ujue nishaachana naye na sina mpango naye, kwanini unaenda kunisemea maneno maneno ya kuniponda.’ Huyo Ali…,” alisema AT.

“Ingawa hakumtaja jina, lakini kwa wakati ule inawezekana kabisa alikuwa Jackline Wolper,” aliongeza.

Kwa upande wake Diamond, akiongea hivi karibuni na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, alikiri kuwa walienda kwenye show hiyo, lakini hakutaka kuzungumza chochote kuhusu kauli ya AT na madai yake.

“Yule ni kaka yangu, alinitangulia kwenye muziki. Huwezi kujua ni kwanini ameamua kusema alichokisema,” alisema Diamond.

AT alisisitiza kuwa Wolper ndiye mrembo wa kwanza maarufu ambaye Diamond alimnasa wakati anaanza kupanda kwenye ngazi za umaarufu katika muziki, lakini alikuwa ametoka mikononi mwa Ali Kiba.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 24, 2017
Video: Hivi ndivyo lilivyojipanga jeshi la polisi Dar katika sikukuu ya Idd El Fitri