Familia ya Mohammed Dewji, imetangaza zawadi ya Sh.1 bilioni kwa mtu yeyote atayetoa taarifa itakayosaidia kupatikana kwa mtoto wao huyo bilionea aliyetekwa Oktoba 11 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Msomaji wa taarifa ya familia hiyo, Azim Dewji amesema leo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umehudhuriwa pia na baba mzazi wa Mo Dewji, Mzee Gullam Hussein.

“Yeyote atakayesaidia kupatikana kwa mtoto wetu mpendwa atazawadiwa Sh. 1 bilioni,” amesema Azim alipokuwa akisoma taarifa hiyo ya familia.

Aidha, amefafanua kuwa taarifa kuhusu alipo zinaweza kutolewa kwa siri kupitia namba za simu ya mkononi, 0755030014, 0717208478 na 0784783228.

Mo Dewji alitekwa majira ya saa 11 alifajiri katika hoteli ya Colloseum iliyoko Osterbay jijini Dar es Salaam na watu ambao jeshi la polisi limesema ni raia wa kigeni (wazungu).

Video: Dau la bilioni 1 latangazwa kupatikana kwa Mo Dewji
Midundo ya Afrika yampagawisha Kanye West