Mbabe wa Kickboxing kutoka Japan, Tenshin Nasukawa amejibu kejeli za mpiganaji wa MMA/UFC, Conor McGregor aliyeonesha kumvunjia heshima baada ya kuona habari kuwa atapigana na Floyd Mayweather.

Conor, ametumia mtandao wa Instagram kumshambulia Mayweather ambaye alimpiga kwa KO katika pambano lao la mwaka jana, akikijeli picha ya kutangaza pambano hilo, inayomuonesha Mayweather akiwa amesimama na Nasukawa.

Katika kejeli zake zilizoambatana na maneno yenye lugha kali, McGregor amekejeli picha hiyo akilifananisha pambano hilo la filamu ya Rush Hour ya Jackie Chan na Chris Tucker, akihoji kama Nasukawa na Jackie Chan.

Nasukawa ambaye hajawahi kushindwa katika mapambano yote 27 ya Kickboxing na mapambano manne ya MMA, alitumia Twitter kumjibu McGregor kwa kutumia lugha safi, akiahidi kuwa atamsaidia kulipiza kisasi cha kipigo alichopokea kutoka kwa Mayweather.

“Hello McGregor, jina langu ni Tenshin Nasukawa. Mimi sio Jackie Chan. Ninaahidi kulipiza kisasi cha kupigwa kwako, tafadhali angalia pambano langu [na Mayweather],” aliandika.

Nasukawa alishinda pambano lake la Septemba dhidi ya mbabe wa UFC, Kyoji Horiguchi.

Katika pambano la kickboxing nchini Japan. Atapigana na Mayweather Disemba 31 itakayofanyika Saitama nchini Japan. Kanuni za pambano hilo bado hazijawekwa wazi.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 7, 2018
Ripoti: Makumi ya wanafunzi walifanya mitihani wakiwa wajawazito