Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa iwapo akitokea mtu yeyote kutaka kuvunja sheria za nchi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Amesema hayo leo, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza kwenye kongamano la Siku ya Demokrasia duniani.

“Haki za binadamu nazo zimetambuliwa katika katiba yetu na nchi yetu imesaini na kuridhia mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu haki za binadamu”.amesema Rais Samia

“Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria ambapo hakuna mtu aliye juu ya sheria, ukivunja sheria basi utashughulikiwa na haichagui yoyote yule”.amesema Rais Samia

“Nchi yetu ina vyama vya siasa takribani 20, tuna vyama vya wafanyakazi, wanataaluma mbalimbali na uhuru wa kukusanyika upo kwa kiasi kikubwa na hii ndio sababu tumeweza kukusanyika hapa kuadhimisha siku ya Demokrasia,” amesema Rais Samia.

Mkurugenzi Kishapu apewa siku saba zahanati ikamilike
Rais Samia: Wanawake tukiiacha nafasi ya urais 2025 Mungu atatulaani