Shirika la ndege Tanzania ATCL kupitia Mkurugenzi wake Mkuu, Ladislaus Matindi limesema kuwa linatarajia kuanzisha safari zake kati ya Uingereza (London) na Tanzania (Dar es salaam).

Ambapo safari hizo zinatarajiwa kufanyika kwa wiki mara tatu katika siku ya Jumatano, Ijumaa na Jumapili kwa kutumia ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Matindi amesema iwapo kutakuwa hakuna mabadiliko yeyote basi safari hizo zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2020 kwani tayari ATCL imepata ratiba yake katika uwanja wa ndege wa Gatwick jijini Londoni huko Uingereza.

Hata hivyo dhumuni kubwa la kuanzisha safari hizo ni baina yao ili kunufaika kichumi kwani kuanzishwa kwa safari hizo kutaleta manufaa makubwa na kuimarisha uhusiano wa muda mrefu.

”Kuna fursa kubwa ya kushirikiana kukuza biashara na uwekezaji kama utalii kupitia ndege ya moja kwa moja, kupitia safari hizo tutaimarisha urafiki wetu na uhusiano wa muda mrefu” amesema Andrew Rosindell ambaye ni Kiongozi wa kamati ya mambo ya nje.

Video: Ukweli kuhusu maziwa ya mama kuongeza nguvu za kiume | Wanaume washauriwa

Naye Mkurugenzi wa biashara wa ATCL, Patrick Ndekana alishukuru Uingereza kwa kutuma ujumbe huo wenye fursa kubwa kwa nchi ya Tanzania.

Maungumzo hayo yamefanyika jana ambapo Uingereza kupitia waziri wake Mkuu ilimtuma mwakilishi kufikisha ujumbe huo nchini.

Aidha, haya ni mapinduzi makubwa kwani mara ya mwisho kutokea kwa safari hizi za moja kwa moja Uingereza na Tanzania ilikuwa mwaka 2000.

Mbali na kuanzishwa kwa safari hizo kwa sasa ATCL inafanya safari nyingine  nje ya nchi ikiwa pamoja na India  (Mumbai), Johannesburg (Afrika ya kusini, Moroni (Koroni), Bujumbura (Burundi), Kampala (Uganda), Lusaka 9Zambia) na Harare (Zimbabwe).

Mifuko mbadala yawaponza maafisa TBS, watumbuliwa
Upinzani wang'aka, 'Hatususii uchaguzi'