Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL limeomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza kwa wateja wao kutokana na upungufu wa ndege zetu kama lilivyowajulisha siku zilizopita.

Kupitia taarifa iliyotolewa katika mtandao wa kijamii, Shirika hilo limesema juhudi zinaendelea kufanyika ili kurudisha huduma kama ilivyokuwa hapo awali huku likijulisha kuwa ndege moja ya Airbus ipo katika hatua za mwisho za marekebisho na inategemewa kurudi katika miruko ya kawaida kuanzia wiki ijayo.

Aidha, ATCL imesema wakati huo huo juhudi zinafanyika ili kupata ndege ya ziada kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya soko katika kipindi hiki cha mwaka chenye uhitaji mkubwa.

Hata hivyo, ATCL imeendelea kuomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza kutokana na mabadiliko ya ratiba, ili kuhakikisha safari zao zinafanyika pamoja na changamoto zilizopo.

Young Africans yawasili Ruangwa kwa kishindo
Watanzania changamkieni fursa China: Balozi Kairuki