Urembo unazidi kuwa ghali mno huku kila mwanadada akifanya lolote kupendeza, walio na matiti madogo huyanenepesha kwa wale wenye makubwa pia huyapunguza na kuwa saizi wanayotaka.

Wanadada wengi wamepoteza maisha kwa kutumia baadhi ya vipodozi katika kujirembesha.

Upasuaji salama wa matiti hugharimu mamilioni ya fedha ambayo wengi wa wanadada hawawezi kugharamu hivyo hulazimika kutumia mbinu zenye bei chee ikiwemo upasuaji ambao hatima yake huwa na athari kubwa maishani mwao.

Jarida la TUKO.co. ke limefanya utafiti na kugundua madhara yanayotokana na upasuaji wa matiti.

1. Matititi huishia kuwa kombo kwa kukosa umbo mzuri.

2. Ngozi huathirika kwa kujikunjakunja.

3. Kovu kuchukua muda mrefu kabla kupona kabisa na kukupa maumivu si haba.

4. Mwili kupasuka na kifaa cha kunenepesha matiti kuonekana nje ya mwili.

5. Kuambukizwa magonjwa mengine ikiwemo kupooza

6. Upasuaji huweza kusababisha kufura kwa ncha ya matiti

7. Huweza kuathiri kwa kupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa

8. Matiti kuanguka – Kwa wengine, badala ya matiti yao kuwa tisti baada ya upasuaji, yanaregarega kama ya ajuza.

9. Rangi ya matiti huweza kubadilika kutokana na kufuja kwa damu wakati wa upasuaji

10. Wengine huathirika kwa kushikwa na upele matitini

11. Matiti huweza kufura na kuwa makubwa kupita kiasi

 

Jambazi Sugu aliyetoroka jela kwa helikopta anaswa
Ali Kiba afuta video ya wimbo wake mpya 'Hela', kisa...