Mtu mmoja jijini Mwanza amekamatwa na jeshi la polisi mara baada ya kujifanya ni daktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) iliyopo jijini Mwanza.

Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) alikamatwa Oktoba 3 mwaka huu baada ya kudaiwa kujifanya daktari bingwa.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wagonjwa waliyo yatoa kwa uongozi wa hospitali hiyo pamoja na jeshi la polisi.

Aidha, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shanna amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na kunaswa akiwa kwenye chumba cha upasuaji na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Amesema kuwa kabla ya kutiwa mbaroni mtuhumiwa huyo alikuwa akijifanya ni daktari bingwa na alifanikiwa kuwatapeli baadhi ya wagonjwa wanaotaka kupata huduma za upasuaji na matibabu kwa njia za mkato kwa kuwatoza kati ya sh. 100,000 na 200,000 ili awapangie tarehe za karibu wapate huduma hizo.

“Jeshi la polisi tulipokea malalamiko ya wagonjwa kutapeliwa na kuibiwa mara kwa mara wodini na hivyo tuliwaelekeza wayafikishe kwa uongozi wa hospitali.tuliweka mtego tukishirikiana na na uogozi wa hospitali hiyo ya rufaa BMC tukafanikiwa kumnasa akiwa kwenye chumba cha upasuaji akiwa amevalia sare  zinazovaliwa na madaktari wakiwa theater,” amesema ACP Shanna.

Hata hivyo, ameongeza kuwa daktari huyo bingwa bandia alipohojiwa alikiri hakuwahi kupata elimu ya taaluma hiyo wala kufanya kazi ya utatibu.

Video: Mama atoa simulizi ya kusikitisha
Man Utd wakanusha kumtimua Jose Mourinho