Klabu ya Atletico Madrid ya Hispania imethibitisha kumsajili beki wa kulia kutoka nchini Colombia Santiago “Santi” Arias Naranjo kwa mkataba wa miaka mitano.

Arias, mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na klabu hiyo ya mjini Madrid-Hispania akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Uholanzi PSV Eindhoven.

Beki huyo alionyesha uwezo mkubwa wakati wa msimu wa 2017/18 na kufanikisha mafanikio ya PSV Eindhoven kutwaa ubingwa wa Uholanzi, huku akiitumikia klabu hiyo katika michezo 173 tangu mwaka 2013.

Atletico Madrid wamethibitisha kumsajili beki huyo, baada ya kumtoa kwa mkopo beki wa kulia Sime Vrsaljko kwenye klabu ya Internazionale (Inter Milan) ya Italia, huku sehemu ya mkataba wa pande hizo mbili ukiruhusu mchezaji huyo kusajiliwa jumla, endapo ataonyesha kiwango kizuri katika ligi ya Italia (Serie A) msimu ujao.

“Baada ya kufanikiwa kuwa sehemu ya kikosi chetu kwa misimu miwli, tumefikia makubaliano ya kumtoa kwa mkopo Vrsaljko kwenye klabu ya Inter Milan, tunamtakia kila la kheri katika changamoto mpya ya soka lake.”

Image result for Sime VrsaljkoSime Vrsaljko

“Baada ya maazimio hayo, tumemsajili beki mwingine Santiago Arias kutoka PSV Eindhovein, ambaye anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Vrsaljko.” Imeeleza taarifa iliyotolewa na Atletico Madrid.

Vrsaljko alikua sehemu ya kikosi cha Croatia kilichofika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia na kufungwa na Ufaransa mabao manne kwa mawili.

Santiago Arias naye alikua sheemu ya kikosi cha Colombia kilichoshiriki fainali za kombe la dunia, kabla ya kutolewa na England katika mchezo wa hatua ya 16 bora. Arias ameshaitumikia timu ya taifa katika michezo 45.

Asante Kotoko kunogesha tamasha la Simba (Simba Day)
LIVE: Mawaziri 11, Makatibu wakuu 14 wakijadili mradi wa umeme wa maji Rufiji