Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kupitia ligi ya nchini Hispania La Liga.

Griezmann ametajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo katika shughuli maalum iliyofanyika usiku wa kumkia hii leo, na kuwabwaga Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Mbali na kumtoa mchezaji bora wa mwaka, pia klabu ya Atletico Madrid imejizolea tuzo nyingine kama ya meneja bora wa mwaka (Diego Simeone), Kipa bora (Jan Oblak) pamoja na beki bora (Diego Godin).

Simeone ametwaa tuzo ya meneja bora wa mwaka kwa kumshinda meneja wa klabu ya Celta Vigo Toto Berizzo pamoja na aliyekua mkuu wa benchi la ufundi la Villarreal  Marcelino.

Tuzo ya kiungo bora wa mwaka imekwenda kwa Luka Modrić wa Real Madrid huku Lionel Messi akishinda tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka.

Wakati huo huo waratibu wa tuzo za mchezaji bora wa mwaka wa La Liga walitangaza kikosi bora cha msimu wa 2015-16 ambapo upande wa mlinda mlango yupo Jan Oblak (Atlético Madrid).

Mabeki: Sergio Ramos (Real Madrid), Diego Godín (Atlético Madrid), Gerard Piqué (Barcelona) pamoja na Marcelo (Real Madrid).

Viungo: Andrés Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona) pamoja na Luka Modrić (Real Madrid).

Washambuliaji: Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Lionel Messi (Barcelona) pamoja na Luis Suárez (Barcelona).

Babu Hans van der Pluijm Anukia Azam Complex
Ligi Ya PL Yaingiza Wanane Tuzo Ya Mchezaji Bora Duniani