Mtoto mwenye umri wa siku mbili amesurika kifo baada ya kutupwa chooni na mama yake mzazi mara baada ya kujifungua, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugumu wa maisha ikiwemo kukataliwa na baba wa mtoto.

Akizungumzia tukio hilo ofisa ustawi wa Jamii halmashauri ya Nsimbo Teresia Mwendapole amesema mtoto huyo baada ya kuokolewa alipelekwa hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi ambapo anaendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi, Ali Makame.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya watoto Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Dokta Maria Matei amethibitisha kumpokea mtoto huyo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake huku akieleza hali ya mtoto huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi, Ali Makame amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari upelelezi umekamilika ikiwa ni pamoja na jalada lake kufikishwa kwa mwendesha mashitaka wa serikali na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.

Dkt. Mpango: Barabara Kabingo - Manyovu kuifungua Kigoma
Azam FC yafuta safari ya Nairobi-Kenya