Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, linamshikilia Lucia Mahazi (42), kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kiume wa siku 2 na kisha kumzika, kwa madai ya kutelekezwa na mwanamume aliyempa ujauzito.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea Mei 26 ambapo wananchi wa eneo hilo waligundua kuwa mwanamke huyo hakuwa na mtoto aliyejifungua Aprili 17, na kuamua kutoa taarifa Polisi.

Magilimba amesema Uchunguzi wa awali ulibaini mama huyo alijifungua April 17 na kumuua April 19, na kumzika katika eneo la shule ya msingi Ididi wilayani Kishapu, majira ya saa 12 jioni wakati mvua kubwa ikinyesha.

Mabaki ya mwili wa marehemu yamekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi, na mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Kigwangalla azindua Filamu ya utalii kwa lugha mbalimbali
Serie A kurejea mwezi Juni