Mtu mmoja ameuawa nchini Venezuela wakati akisubiri kupiga kura ya maoni liliyoandaliwa na upinzani dhidi ya mipango ya Serikali kuandika upya katiba ya nchi hiyo ili iweze kuendana na wakati.

Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wamewashambulia wapiga kura nje ya kituo cha kupigia kura nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Caracas, huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali.

Aidha, Mpaka sasa idadi kubwa ya watu wamefariki dunia katika ghasia ambazo zimeelezwa kuwa ni mbaya zaidi kutokea nchini humo na zimeathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo na jitihada za Rais  Nicolas Maduro kung’ang’ania madarakani.

 

 

Roger Federer aweka historia Wimbledon
Hawa wa Diamond hoi kwa gongo, atamani angekuwa Zari

Comments

comments