Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kukatana mapanga na kuchomana visu katika ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi katika kitongoji cha kireneo wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa Mara, Juma Ndaki ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana asubuhi katika Kitongoji cha Kireneo wilaya ya Serengeti mkoani humo.

Amemtaja aliyefariki kuwa ni Kibure Samweli (39) ambaye alichomwa kisu tumboni na kifuani, wakati Nyang’anyi Waitara (44) mkazi wa Itununu katika tukio hilo alikatwa kwenye mkono.

Amesema kuwa chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa kimapenzi kwani mwanamke aliyekuwa ameolewa na Nyang’anyi Waitara sasa ni mke wa Munge.

Aidha, Munge Samweli ambaye ni kaka wa marehemu alikatwa pajani na mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akiwashambulia.

“Aliyekufa ni mdogo wake Munge ambaye alifika kwenye tukio hilo na kumkuta kaka yake wakishambuliana na Waitara ndipo alipochukua panga na kuanza kumsaidia kaka yake ndipo Waitara alipomchoma kisu tumboni na kifuani,”amesema Kamanda Ndaki

 

 

 

Rais JPM afanya uteuzi wa nafasi 9
Mwalimu wa Chuo asitishwa kazi kwa kumtaka kimapenzi mwanafunzi