Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang kwa mara ya kwanza amekiri palifanyika mazungumzo ya kutaka kuihama klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Manchester City wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyo alikua gumzo wakati huo wa usajili kufuatia juhudi kubwa aliyoionyesha msimu uliopita ya kufunga mabao 39 katika michezo ya michuano yote aliyocheza, akiwa na klabu ya wa Borussia Dortmund.

Aubameyang mwenye umri wa miaka 27 amefichua siri hiyo alipofanyiwa mahojiano maalum na jarida la Onze Mondial la nchini Ufaransa, ambapo amesema wakala wake ambaye ni baba yake mzazi alijaribu kufanya mazungumzo ya Man city lakini mambo yalikwenda divyo sivyo, baada ya uongozi wa Borussia Dortmund kukataa kushiriki katika mpango huo.

Mbali na klabu ya Man city, pia mshambuliaji huyo raia wa nchini Gabon alikua anahusishwa na taarifa za kuwatakiwa na klabu za Real Madrid na Paris St-Germain.

Majaliwa apokea sh. mil. 5 kwa ajili ya waathirika wa tetemeko Kagera
Wafanyakazi wakala wa ufundi na umeme Temesa watakiwa kufanya kazi kwa bidii