Mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid imejikuta katika wakati mgumu wa kuihitaji huduma ya mshambuliaji kutoka nchini Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, kufuatia klabu ya Manchester City kuingia katika harakati za ushindani.

Manchester City waliripotiwa kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Borussia Dortmund kwa ajili ya usajili wa Aubameyang wakati wa usajili wa majira ya kiangazi huku kiasi cha 65 kilitajwa kama nyenzo ya kufanikisha hatua hiyo, lakini mambo yalikwenda mrama.

Pamoja na taratibu hizo za Man City, bado mabingwa hao wa barani Ulaya wameendelea na mikakati ya kutaka kumng’oa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye aliwahi kusema hadharani suala la kutamani kuichezea Real Madrid.

Hatua hiyo inatajwa kuongeza morari kwa viongozi wa Real Madrid kwa kuamini mambo yatakua sawasawa mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo inadhaniwa kuwa, safari ya Real Madrid ya kuelekea mjini Dortmund nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund, kutamuwezesha Zinedine Zidane kusisitiza mpango wa usajili wa Aubameyang.

Mchezo huo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya umepangwa kuchezwa hii leo.

Aubameyang alionyesha makali ya kupachika mabao 36 katika michezo 45 aliocheza msimu uliopita.

Video: JPM afichua madudu Bandari ya Dar es salaam
Juan Mata Athibitisha Kwa Vitendo, Mourinho Amkubali