Meneja wa Washika Bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal FC) Mikel Arteta amesema kuna ishara njema kwa mshambuliaji wake kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kusaini mkataba mpya.

Mkataba wa nahodha na mshambuliaji huyo wa kikosi cha Gabon ndani ya Arsenal unatamalizika mwishoni mwa Juni mwakani 2021, ambapo Arteta amesema The Gunners imeshamwambia kwa nini aendelee kubakia Emirates.

“Amesema anahitaji kuthaminiwa, nasi tupo tayari kumthamini kama mchezaji wetu”. Alisema Mikel Arteta.

Aubameyang, ameshafunga mabao 61 katika michezo 97 aliyocheza tangu alipojiunga na Arsenal 2018 akitokea Borrusia Dortmund.

Arteta aliongeza kwa kusema: “Nadhani kwa muda huu ni furaha kubwa juu yake, furaha hii inakuja kwa sababu ameanza kujituma na kuwa na furaha anapokuwa mazoezini”.

Mwezi Machi mwaka huu, kabla ya ligi haijasimama kutokana na janga la virusi vya Corona Meneja Arteta alisema atahakikisha anambakiza Aubameyang kwa njia yoyote ile na klabu kumpa kandarasi nyingine mpya.

Klabu za FC Barcelona na Inter Milan tayari zimeshaonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Arsenal, inakamata nafasi ya tisa kwenye msimamo wa EPL watasafiri siku ya kesho Jumatano kukutana na mabingwa watetezi Manchester City kwenye mechi kiporo ikiwa ni sehemu ya kurudi ligi baada ya kusimama kwa zaidi ya siku 90.

JPM atahadharisha kampeni za matusi, awashukuru wapinzani
BREAKING NEWS: Rais Magufuli aagiza shule zote kufunguliwa Juni 29