Nahodha na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ameelezea masikitiko yake, kufuatia kushindwa kuisaidia The Gunners kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League.

Arsenal walifungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Olimpiacos ya Ugiriki usiku wa kuamkia leo jijini London, na kuondoshwa kwenye michuano hiyo kwa sheria ya bao la ugenini, kufuatiamchezo wa kwanza kushuhudia The Gunners wakiibuka naushindi wa  bao moja kwa sifuri.

Licha ya kufunga bao la kusawazisha, Aubameyang alikuwa kwenye nafasi nzuri ya walau kuweka hai matumaini ya washika mitutu hao wa London kusonga mbele muda mchache kabla ya mchezo kumalizika, lakini akajikuta akipoteza nafasi hiyo ya wazi.

Baada ya tukio hilo, mshambuliaji huyo kutoka Gabon alionekana kuziba uso wake kama ishara ya kujutia kilichotokea huku ukimya ukitawala kwa mashabiki wa Arsenal waliojitokeza kwenye mchezo huo.

“Nimehuzunika na kilichotokea hicho ndicho ninachoweza kusema. Ni ngumu na imenigusa,” alisema Aubameyang.

“Nadhani tulipoteana hilo limetugharimu katika huu mchezo, hatukuwa na bahati. Kilichopo ni kujaribu kuhamishia nguvu zetu kwenye ligi.”

Mshambuliaji kutoka Morocco Youssef El-Arabi alikua mwiba kwa Arsenal waliokua nyumbani jijini London, baada ya kufunga bao la pili kwa Olympiacos dakika ya 120, ndani ya dakika 90 za kawaida washika mitutu wa London walifungwa bao moja hivyo ilibidi wakaamuliwe dakika 30 kwani mchezo wa kwanza, walishinda bao 1-0 nchini Ugiriki.

Aubameyang, msimu uliopita alitwaa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa msimu wa Ligi Kuu England ‘EPL’ sambamba washambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah na Sadio Mane, kila mmoja akipachika mabao 22.

Mafua yamuandama papa Francis
Membe afukuzwa uanachama CCM, Makamba asamehehewa