Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ameeleza hisia zake za kutaka kucheza soka akiwa na kikosi cha mabingwa wa soka nchini England (Chelsea).

Hisia za mshambuliaji huyo zimefichuliwa na gazeti la The Sun, ambalo mapema hii leo limetoka na taarifa zinazohusu mipango ya Aubameyang ya kuhitaji kucheza soka nchini England.

The Sun wamedai kuwa mara kadhaa, mshambuliaji huyo amenukuliwa na watu wakewa karibu akisema anatamani sana kucheza kwenye klabu ya Chelsea, kutokana naumahiri wa kikosi cha klabu hiyo ambayo msimu uliopita ilifanya vyema kwenye ligi yanchini humo, na kutwaa ubingwa wa PL.

Wakati Aubameyang akitamani kujiunga na The Blues, meneja wa klabu hiyo Antonio Conte hana habari nae kwa sasa, zaidi ya kumfikiria mshambuliaji kutoka nchiniHispania na klabu ya Real Madrid Alvaro Morata ambaye anamuhitaji kama mbadalawa Diego Costa.

Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon lakini ni mzaliwa wa Ufaransa, kwa sasa yupo mashariki ya kati sambamba na kikosi cha klabu yake ya Dortmund kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi ya Ujerumani ambayo itaanza mwezi ujao.

Hata hivyo klabu za AC Milan na Paris Saint-Germain zimeonyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili Aubameyang na huenda zikatuma ofa ya usajili kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi ujao.

 

Florentino Perez aweka wazi anavyomhusudu Eden Hazard
Kisela yaikimbiza wasikudanganye na Eneka ya Diamond