Nahodha na Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang huenda akaondoka mwezi Januari 2022, baada ya kufanya mazungumzo na wakala wake.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Gabon ana wakati mgumu wa kurejesha imani kwa Mashabiki wa Arsenal, kufuatia mwenendo wake kutokua wa kuridhisha msimu huu 2021/22.

Inaelezwa kuwa Aubameyang amemuomba wakala wake kumtafutia klabu ya kuitumikia kuanzia mwezi Januari mwaka 2022, kutokana na kukosa furaha ndani ya Arsenal.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa, tayari wakala wake ameanza mpango wa kuzungumza na Uongozi wa FC BArcelona ya Hispania ili kuangalia uwezekano wa mteja wake kujiunga na klabu hiyo.

FC Barcelona watalazimika kufanya usajili wa Mshambuliaji wakati wa Dirisha Dogo la Usajili, ili kuziba nafasi ya Kun Aguero ambaye Afya yake haiko vizuri.

FC Barcelona waliwahi kuhusishwa na mpango wa kumsajili Aubameyang msimu uliopita, lakini Mshambuliaji huyo alifanya maamuzi ya kusaini mkataba mpya na Arsenal ambao utadumu hadi mwaka 2023.

Tangu amejiunga na Arsenal mwaka 2018, Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang ameshaifungia klabu hiyo ya Kaskazini mwa London mabao 68 katika michezo 128 aliyocheza.

Mayele atamba kuifunga Simba SC Jumamosi
Moto walipuka Gerezani, wahofiwa kuua wafungwa