Kiungo kutoka nchini Uganda Khalid Aucho amekanusha taarifa za kuwa mbioni kuondoka Young Africans na kuelekea kwingine mara baada ya Mkataba wake utakapofikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Aucho alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea El Makkasa ya nchini Misri, na amekua muhimili mkubwa katika safu ya kiungo klabuni hapo.

Kiungo huyo amesema ameshangazwa na taarifa zilizotolewa mwishoni mwa juma lililopita na moja ya chombo cha habari, kikieleza amegomea mkataba mpya Young Africans na yupo tayari kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Amesema suala hilo halina ukweli na huenda liliandaliwa kwa ajili ya kuwavuruga Mashabiki wake na wale wa Young Africans ambao wamekua na furaha ya kuiona timu yao ikifanya vizuri ndani na nje ya Uwanja.

“Nimeshangazwa na taarifa za mimi kugomea mkataba Young Africans, ukweli ni kwamba hizo taarifa sio za kweli, nipo katika mazungumzo na Uongozi na yanaendelea vizuri tu,”

“Labda niweke wazi kuwa kwa hivi sasa sifikirii na sina mpango wa kuondoka Young Africans, kwani bado nina mengi ya kufanya hapa.”

“Mashabiki wangu na wa klabu ya Young Africans kwa ujumla naomba mpuuze taarifa zilizotolewa dhidi yangu siku chache zilizopita, binafsi nipo hapa kwa sababu ninajua ninachokifanya na ninaipenda kazi yanga hapa.” amesema Aucho

Wachezaji wengine ambao wapo katika mazungumzo na Uongozi wa Young Africans ili kufanikisha mpango wa kusaini mkataba mpya ni Djigui Diara, Dickson Job na Jesus Moloko.

Kampuni ya Kilombero yaibuka kidedea tuzo za ATE 2022
KFA yakanusha kujiuzulu kwa Paulo Bento