Kiungo kutoka nchini Uganda na klabu ya Young Africans Khalid Aucho amekanusha taarifa zinazomuandama kwa sasa, zikidai yupo njiani kuachama na klabu hiyo.

Aucho ameonekana kuwa nguzo imara katika nafasi ya kiungo kwenye kikosi cha Young Africans tangu alipotua klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo ambaye pia ni Nahodha Msaidizi wa kikosi cha Uganda amesema taarfa za kuhusishwa na mpango wa kuachana na Young Africans wakati wa dirisha dogo amezisikia, na amezipuuza kutokana na kuamini hana pakwenda zaidi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

“Sina mpango wa kwenda kokote, mimi bado ni mchezaji wa Yanga,” amesema Aucho kwa kifupi.

Khalid Aucho alisajiliwa Young Africans akitokea nchini Misri alipokua akiitumikia klabu ya El Makkasa ambayo alimsajili kuanzia mwaka 2019–2021.

Young Africans kumuuza Aucho
Almasi Kasongo amaliza utata PENATI ya Young Africans