Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye anafahamika kwa kutoa kauli ‘tata’, amefyatuka tena akimshauri Rais John Magufuli kuihama CCM endapo kile alichokiita ‘njama alizozibaini’ ndani ya chama hicho zitaletwa mezani.

Gwajima ambaye amekiri kuwa katika kampeni alikuwa hamkubali Dk. Magufuli kutokana na kutokuwa na imani na CCM, amesema amemkubali  sana baada ya kuanza kazi ya urais kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua ndani ya muda mfupi.

Akizungumza katika ibada ya Jumapili kanisani kwake, Gwajima ameeleza kuwa amebaini njama za baadhi ya wanachama wa CCM ambao ‘dili’ zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘flow meter’ ya mafuta yaingiayo nchini na makontena yaliyokamatwa yalikuwa yanawahusu, wameanza kampeni ya chinichini nchi nzima kutaka Rais Magufuli asipewe uenyekiti wa chama hicho.

Amesema kuwa watu hao wanazunguka nchi nzima kuwashawishi wanachama wa CCM kuridhia hoja ya kutenga uenyekiti wa chama na urais, ili kumnyima nafasi hiyo Rais Magufuli ambaye utendaji wake umewabana bila kujali ni wa chama chake.

Hivyo, amemshauri Rais Magufuli kuwa endapo itatokea hilo, akihame chama hicho na kuendelea na kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mengine, msikilize mwenyewe hapo chini:

Video: Ahadi ya Makamu wa Rais kuhusu ujenzi wa barabara Tunduru imefika Bungeni
Magaidi wa ISIS watajwa mauaji ya watu 50 Marekani