Jay Z ameiongezea nguvu ngoma kubwa ya Fat Joe na Remmy Ma iliyobatizwa jina la ‘All The Way Up’ baada ya kushiriki katika ‘Remix’ rasmi ya wimbo huo.

Jigga amefanya ‘verse’ moja nzima akizungumzia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na album mpya ya mkewe Beyonce, Lemonade. Mwingine aliyesikika kwenye wimbo huo ni French Montana ambaye alikuwepo pia kwenye ile ya awali.

Ngoma hiyo imeachiwa kwa upekee kupitia mtandao wa Tidal anaoumiliki rapa huyo nguli pamoja na wasanii wengine wakubwa. Mradi huo mkubwa umewekwa wazi ikiwa ni siku chache baada ya Fat Joe kupiga picha na Jay Z nyuma ya jukwaa kwenye show kubwa ya ziara ya Beyonce ya ‘Formation World Tour’.

NY Giants: Crack – Hov #formationtour #allthewayup

A photo posted by FAT JOE (@fatjoe) on

Baada ya miaka kadhaa ya kutoelewana, marapa hao nguli kutoka mitaa ya jiji la New York wameweka kando tofauti zao na kupakua mzigo. Mwaka 2014, Fat Joe aliweka kando tofauti kati yake na 50 Cent na kuachia ngoma ya pamoja iliyoitwa ‘Free Again’.

Unaweza kuusikiliza hapa

TASWA Wakutana Na Kujadili Mambo Matatu
Tajiri Wa Paris Saint-Germain Amtengea Fungu La Pesa Ronaldo

Comments

comments