Siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuwataka chadema kutothubutu kuandamana na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kutikisa kiberiti cha gesi, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amejibu katazo hilo.

Waziri Nchemba alisema kuwa kama wapinzani walikuwa wamezoea kutikisa kiberiti, wanapaswa kusitisha mara moja kwani wakati huu ni tofauti na wanachofanya ni kutikisa kiberiti cha gesi.

Akijibu maelezo ya Nchemba, Lema amedai kuwa chama chao hakijaribu na kwamba Operesheni UKUTA iko palepale Septemba 1.

Amesema kuwa wanafanya maandamano hayo kwa sababu wanasaka haki yao ya kikatiba. Lema amezungumzia pia picha zinazoonekana kwenye vyombo vya habari ikionesha Polisi wakiwa katika maandalizi ya kupambana na uhalifu, wakilenga zaidi kupambana na operesheni Ukuta.

Askari wa Upelelezi auawa Baa, 6 Wakamatwa
Serikali yaanza kupeleka fedha za miradi katika Halmashauri, “Fedha hii tafadhali ni ya moto"