Mfalme wa RnB, R.Kelly amembariki mwimbaji wa Nigeria, Davido kwa kufanya remix ya wimbo wake ‘If’ aliouachia hivi karibuni.

Kelly ambaye wiki iliyopita aliweka kwenye mitandao ya kijamii kionjo cha remix ya wimbo huo, amesikika kwenye sehemu kubwa zaidi ya wimbo huo wenye dakika 4.

Ndani ya remix hiyo ya dakika 4 ambayo imeendelea kutunza mdundo na sehemu ya wimbo wa Davido, R. Kelly anaanza kusikika kwenye ufunguzi (intro), kisha anaachia shairi la Davido, kabla ya kurudi na kuua kwenye dakika moja na sekunde nne. Mwisho, anamuachia Davido aendelee kumuimbia mpenzi wake Brigette huku Sauti ya R.Kelly akitambaa kwa chini.

Remix hiyo inaipa nguvu kubwa zaidi ‘If’ ya Davido ambayo tayari imeangaliwa zaidi ya mara milioni 14 kwenye YouTube, huku ikishika nafasi za juu kwenye vituo vya redio na runinga katika kona mbalimbali duniani.

Video: Manji adaiwa kukamatwa tena, Mchongo wa Escrow
Mugabe achangia ng'ombe kwa Umoja wa Afrika kuondoa utegemezi