Msanii aliye chini ya label ya ‘WCB’, Raymond ameeleza jinsi alivyoweza kushiriki kuzing’arisha ngoma kubwa na mashairi ya Boss wa label hiyo, Diamond Platinumz.

Mkali huyo kutoka Mbeya ameiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm kuwa ameshiriki kuandaa baadhi ya hits na kumpa ‘melodies’ Diamond ikiwa ni pamoja na katika verse ya ‘Zigo Remix’ aliyoshirikishwa na AY pamoja na ‘Make Me Sing’ aliyoshirikishwa na AKA wa Afrika Kusini.

Alisema kuwa Diamond ni msanii mwenye sauti nyingi za kulalamika kwahiyo baada ya kusikia mdundo wa ‘Zigo Remix’ alimuomba kusaidia kupata sauti zenye ladha ya uchizi kwa mbali (crazy) ili kuung’arisha.

Mbali na ngoma hizo, Raymond ameeleza kuwa alishiriki kwa kiasi kikubwa kuandika wimbo wa ‘My Life’ wa Dogo Janja ambao ulimrudisha vizuri msanii huyo wa Ngarenaro.

Kwa mujibu wa Raymond, ushirikiano huo kwenye labe ya WBC ni suala endelevu kwani yeye pia alisaidiwa na Diamond kuandika mashairi na sauti za wimbo wake ‘Kwetu’ lakini pia Harmonizer alishiriki katika wimbo wake mpya wa ‘Natafuta Kiki’.

Sikiliza hapa:

Wapinzani wasusia Bunge, wapanga haya dhidi ya Naibu Spika
Chris Brown afyatuka baada ya shabiki kumshtaki kwa wizi wa ‘Kofia’

Comments

comments