Ikiwa leo ni siku ambayo inatimia miaka mitatu tangu alipofariki mfalme wa mitindo huru, Albert ‘Ngwair’ Mangweha ambaye uwezo wake ulikuwa wa kipekee, DJ K-U amefanya mchanganyiko wa aina yake wa baadhi ya nyimbo kubwa za msanii huyo alioupa jina la ‘Its all about Ngwair’.

Katika mchanganyiko huu wa dakika takribani 55 aliouwasilisha kwa Dar24, ni dhahiri kwamba heshima ya Ngwair itaendelea kubaki kwenye muziki wa Tanzania kwa vizazi vingi vijavyo na hata wewe utaizidisha mara dufu heshima uliyokuwa naye kwake.

Ngwair alifariki Mei 28, 2013 alipokuwa Johannesburg nchini Afrika Kusini. Jina lake halitafutika kwenye ramani ya muziki wa Tanzania.

Apumzike kwa amani. Amina!

Nape: Kuna mambo najifunza kwa Lowassa
Kenya Washtushwa Na Kasi Ya Timu Ya Vijana Ya Tanzania

Comments

comments