August Alsina amefunga ukurasa wa tofauti kati yake na mama yake mzazi, Sheila Blair akiwa kwenye jukwaa la ziara yake ya kimuziki.

Alsina ambaye anaendelea na ziara yake ya ‘Don’t Matter’ alimpandisha jukwaani mama yake mzazi siku ya Jumamosi, akampigia magoti huku ukisikika wimbo wa ‘Make It Home’.

Katika wimbo huo, Alsina anamueleza mpenzi wake jinsi ambavyo anahangaika na dunia kutafuta maisha lakini anataka kurudi nyumbani. Anamueleza kuwa kama hatafanikiwa kufika nyumbani amueleze mama yake kuwa ‘anampenda’ huku ujumbe mwingine akiulekeza kwa wadogo zake.

Mama yake Alsina, Sheila aliweka ujumbe kwenye Instagram pamoja na kipande cha video kinachoonesha tukio la kumaliza tofauti na mwanae baada ya miaka miwili ya mtafaruku wa kifamilia.

“Katika kuteseka kwangu kwa takribani miaka miwili bila kufahamu kitu ambacho Mungu alikuwa akifanya kwenye maisha yangu. Namshukuru Mungu kwa maumivu niliyokuwa nayo ambayo yamesababisha nitafute njia ya kupata pumziko ndani yake,” tafsiri isiyo rasmi ya alichoandika Sheila.

Aliongeza kuwa anmshukuru Mungu kwa kuwezesha kurejesha umoja wao kama familia na kuwafanya kuiona tena thamani ya upendo na familia.

Alsina aliwahi kuweka wazi kuwa hana uhusiano mzuri na mama yake na kwamba ilikuwa inaweza kupita hata miezi kadhaa hawajawahi kuzungumza. Pia, alikosoa hatua ya mama yake huyo kuwa anajibu masuala ya mgogoro wa kifamilia kupitia mitandao ya kijamii badala ya kumuita yeye kama mtoto wake na kuzungumza naye.

DJ D- Ommy azidi kuwa ‘Wakimataifa’, ashirikiana na DJ Walshy Fire wa Jamaica
Aliyefunga ndoa na Laptop yake aiburuza serikali mahakamani, Jaji aridhia…