Mkali wa RnB, August Alsina ameweka wazi kuwa ingawa anatembea na anaonekana mwenye afya, anaumwa wakati wote aliowahi kuugua na kwamba chanzo ni tatizo la ini linalomtafuna.

Alsina mwenye umri wa miaka 24, amefunguka jana alipokuwa akizungumza kwenye ‘talk show’ na Jada Pinkett-Smith, huku akieleza kuwa hataki kulizungumzia sana kwa sababu hatafuti huruma ya mtu yoyote.

“Nina ugonjwa wa ini. Mfumo wa mwili wangu unapambana wenyewe. Ukweli ni kwamba naumwa wakati wote,” alisema. “Sipendi kulizungumzia sana hili kwa sababu sihitaji huruma ya mtu yoyote. Naomba msinichukulie kama mgonjwa wa saratani kwa sababu sio ugonjwa unaonikabili,” aliongeza.

Tamko hilo la Alsina limerudisha kumbukumbu nyuma ambapo mwaka 2014 aliwahi kupoteza fahamu kwa takribani siku tatu baada ya kuanguka akiwa jukwaani jijini New york na kulazwa hospitalini. Lakini alirejea na kuendelea na ziara yake akiambatana na Usher Raymond na Chris Brown.

Mwaka 2015, aliweka wazi kuwa anapoteza uwezo wa kuona lakini bado aliendelea kupiga kazi. Mwanamukizi huyo kutoka New Orleans aliachia LP (Long Playing) albam yake ‘This Thing Called Life’ ikiwa ni maandalizi ya albam yake rasmi aliyoibatiza jina la ‘DRUGS’ inayotarajiwa kuingia sokoni mwaka huu.

 

Video: Simanzi kifo ghafla babu nembo ya taifa, Polisi kufumuliwa
Mayweather aponda muziki wa Rap, awachana marapa wa sasa