Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) nchini Godfrey Chibulunje amesema bei ya mafuta ya Taa, Petrol na Dizeli zimepungua kwa baadhi ya Mikoa.

Mamlaka hiyo imesema kuwa bei za jumla na rejareja za mafuta yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Aprili 2020.

Amesainisha bei ya Petroli imepungua kwa Tsh. 219/lita (sawa na 10.5%), Dizeli Tsh. 143/lita (sawa na 7.17%) na mafuta ya taa yakipungua kwa Tsh 355/lita (sawa na 18.47%).

Ambapo katika mkoa wa Dar es Salaam bai ya rejareja kwa Petroli inauzwa kwa Tsh.1,868, Dizeli kwa Tsh. 1,846 na mafuta ya taa kwa Tsh. 1,568.

Huku bei za jumla Petroli imepungua kwa Tsh. 218.59/lita (sawa na 11.14%), Dizeli kwa Tsh. 142.25/lita (sawa na 7.63%) na Mafuta ya Taa zimepungua kwa kwa Tsh. 354.09/lita (sawa na 19.69%).

Ameongeza kuwa Mei 2020, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini (yaani Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara) zimepungua kwa Tsh. 463/lita(sawa na 21.88%) na Tsh. 377/lita (sawa na 18.21%).

Aliyetangazwa kufa 2016 bado yuhai
Man Utd yawaita walio nje ya England