Kijana mdogo raia wa Australia amekuwa  mtu wa kwanza mdogo zaidi kuliko wote duniani kwa umri  kuendesha ndege yenye injini moja.akiwa na umri wa miaka kumi na minane tu , Lachlan Smart ni mdogo kwa mwaka mmoja chini ya raia wa Marekani aliyekua akishikilia rekodi hiyo ya dunia.

Bw Smart alitumia muda wa takriban miezi miwili kukamilisha safari yake, ambapo aliweza kutua katika viwanja ishirini na vinne.

baada ya kurejea kwenye uwanja wa ndege wa Queensland ambako alianzia safari yake , kijana huyo alisema anachotamani ni kulala kwenye kitanda chake tena kwani alikuwa na safari ndefu.

Jeshi La Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam Laongeza Nguvu Operesheni Ya Vikindu,La peleka Askali Wengine 80,Taarifa Kamili Kutolewa Jumanne
Jenister Mhagama Azindua Taasisi Ya Ujasiliamali Na Ushindani Tanzania(TEEC)