Serikali ya Australia imetangaza kuwa imepania kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa bangi duniani kwa ajili ya matumizi ya matibabu.

Taifa hilo limepanga kufanya mabadiliko katika sheria zake na kujiunga na Canada na Uholnazi ambazo kwa sasa ndizo nchi pekee duniani ambazo huuza bangi nje ya nchi.

Aidha, Waziri wa Afya nchini humo, Greg Hunt amesema hatua hiyo itawasaidia pia wagonjwa wengi nchini Australia kuweza kutibu maradhi yao.

“Lengo letu liko wazi, kuwapa wakulima na wenye viwanda wa Australia nafasi bora zaidi katika kuwa wauzaji nambari moja wa bangi ya kutumiwa kwa sababu za kimatibabu duniani,”amesema Hunt

Hata hivyo, inasemekana kuwa thamani ya biashara ya bangi duniani huenda ikafikia $55bn (£40bn; A$70bn) kufikia mwaka 2025, kwa mujibu wa makadirio ya kampuni ya Marekani ya Grand View Research.

 

Majaliwa ahimiza kilimo cha Kahawa
Video: Lissu adai alishambuliwa kisiasa