Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limepambana na watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi waliokuwa na nia ya kutekeleza tukio la uhalifu nyumbani kwa mfanyabiashara mkazi wa mji wa Vwawa wilayani Mbozi, ambapo katika majibizano ya risasi mtu mmoja amefariki dunia.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe (RPC), Mathius Nyange ambapo amesema kuwa  baada ya kumpekua jambazi huyo wamemkuta na silaha tatu ikiwemo bunduki na risasi 3, upanga na kifaa cha kisasa kinachotumika kumzimisha mtu fahamu wakati wa kufanya tukio.

Aidha, kufuatia tukio hilo wakazi wa mkoa wa Songwe wamelishauri jeshi la polisi kuhakikisha usalama wa raia wanaothubutu kutoa taarifa kwa jeshi hilo zinazohusu wahalifu na kusisitiza elimu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi iimarishwe ili wananchi washiriki ipasavyo kutokomeza matukio ya uhalifu

Hata hivyo, Kamanda Nyange amesema kuwa Mkoa wa Songwe sio mahali salama kwa watu wanofanya uhalifu na kuongeza kuwa wakija hawatarudi salama kwakuwa ulinzi ni wa kutosha hivyo wasidiriki kuhatarisha wananchi na mali zao.

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 22, 2017
Zitto: Bunge limezidi kusimangwa na serikali