Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ruaruke Wilayani Kibiti Mkoani Pwani, Ramadhani Mzurui ameuwa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo huku mke wake akijeruhiwa na watu wasiojulikana.

Aidha, Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mchukwi Dkt. Emmanueli Humbi amedhibitisha kupokelewa kwa mwanamke aliyejeriwa kwa risasi na kusema kuwa yupo katika chumba cha matibabu ya dharura.

Hata hivyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema kuwa tayari polisi wameshakwenda eneo la tukio kwaajili ya uchunguzi zaidi ili kuweza kuwabaini watu waliohusika na tukio hilo

Halima Mdee aachiwa kwa dhamana
Video: Ngeleja ajisalimisha Serikalini, arejesha mamilioni ya Escrow