Watu 19 wameripotiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu na wengine 45 kujeruhiwa baada ya mtu mmoja asiyefahamika kuvamia kituo cha kusaidia watu wenye ulemavu mbalimbali katika eneo la Sagamihara nje kidogo ya jiji la Tokyo nchini Japan, akiwa na kisu.

Mshambuliaji huyo alitekeleza tukio hilo baya majira ya saa nane na nusu usiku kwa saa za chini humo. Wakaazi wa eneo hilo wameeleza kuwa walimuona awali mtu huyo akiwa katika viunga vya eneo hilo na kisu kikubwa mkononi mwake.

Asahi Shimbun imeripoti kuwa polisi wanamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 26 ambaye alijipeleka katika kituo cha polisi na kusema “nimefanya”. Imeelezwa kuwa baada ya kuhojiwa, mtu huyo alikaririwa akisema, “Nataka kuwaondoa kwenye dunia hii watu wenye ulemavu.”

Steering ya gari la muuaji aliyejisalimisha polisi

Steering ya gari la muuaji aliyejisalimisha polisi

Afrika Kuwa Na Timu Saba Fainali Za Kombe La Dunia 2026
Paul Pogba Awachanganya Mashabiki Wa Man Utd