Meneja mpya wa klabu ya Shanghai SIPG Andre Villas-Boas anaangalia uwezekano wa kumsajili beki na nahodha wa kikosi cha Chelsea John Terry.

Gazeti la The Daily Express la nchini England limeeleza kuwa, Terry mwenye umri wa miaka 35, huenda akajiunga na AVB ambaye aliwahi kupita Chelsea kama mkuu wa benchi la ufundi.

Beki huyo ana nafasi kubwa ya kuondoka wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia changamoto inayomkabili katika kikosi cha The Blues ya kuwania nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Meneja wa sasa wa Chelsea Antonio Conte ameonyesha kutomuamini sana Terry, kama ilivyokua kwa mameneja waliopita, jambo ambalo limekua kikwazo kwa beki huyo kufikia lengo la kucheza mara kwa mara.

Wakati wa utawala wa AVB, Terry alikua anacheza katika kikosi cha kwanza wakati wote, na alionyesha kuwa muhimili mkubwa kwenye safu ya ulinzi, jambo ambalo meneja huyo kutoka nchini Ureno anaamini bado litamsaidia katika mipango yake akiwa na Shanghai SIPG ya nchini China.

AVB mwenye umri wa miaka 39 alitimuliwa Stamford Bridge baada ya miezi minane, kufuatia matokeo mabovu yaliyokua yakimuandama katika msimu wa 2011–2012.

Meya aliyeshiriki kumfananisha mke wa Obama na Sokwe ‘ajitumbua’
#HapoKale