Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva ameteua kamati ya maendeleo ya ujenzi wa uwanja Bunju complex.

Kazi kubwa ya kamati hiyo itakuwa kuratibu shughuli zote za ujenzi wa uwanja ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha za ujenzi wa uwanja huo unaotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni.

Katika uteuzi huo rais Aveva amemtua cpt mstaafu wa jeshi na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Simba.Zacharia Hans Pope kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo huku Salim Muhene akiteuliwa kuwa makamu wa mwenyekiti.

Muhene pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu.

Kwenye uteuzi huo wajumbe watakuwa Ally suru.ambae nae ni mjumbe wa kamati ya utendaji.Adam Mgoi ambae pia ni mdhamini wa klabu.

Cressenteus Magori.Imani Kajura.Gerry Ambi.Pamoja na Issa Batenga ambae pia atakuwa katibu wa kamati hiyo.

Katika hatua nyingine kamati hiyo itakutana hivi karibuni na waandishi wa habari kuelezea masuala mbali mbali yanayohus

Imetolewa na

Haji S.Manara

Mkuu wa habari wa klabu ya Simba.

Maimartha amtolea uvivu Ray C
Katibu Mkuu Mpya wa Chadema ampima Dk Slaa