Kesi inayo wakabili viongozi wa klabu ya Simba Evans Aveva  na Geofrey Nyange kaburu, imetajwa  tena hii Leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam.

Jopo la mawakili wa upande wa jamuhuri  likiongozwa na Leonard Swai  limesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Aveva na Kaburu walifikishwa mahakamani hapo Julai 3 mwaka huu na kusomewa mashtaka 5 yakiwemo ya kujilipa madeni ya  kiasi cha dola 300,000 na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Oktoba 11 mwaka huu, na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande.

 

Mashabiki wa soka Zanzibar waushutumu uongozi wa ZFA
FBI yafichua muuaji wa Las Vegas alivyojipanga, wamnasa mpenzi wake