Rais wa klabu ya Simba amewaomba radhi mashabiki, wanachama pamoja na wapenzi wa klabu hiyo nchini kufuatia kwa timu yao kutofanya vizuri na kushindwa kufikia malengo katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara.

  • RAIS WA SIMBA SC AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

Rais wa klabu hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano Collosseum Hotel Bw. Evance Aveva amesema kuwa matokeo mabaya ya timu ya Simba kwa msimu huu wa ligi kuu hayajasababishwa na uongozi kama jinsi maneno yanavyozagaa na kuongeza kwamba uongozi umejitahidi kutimiza mahitaji yote kwa wachezaji wao.

Akitaja sababu mbalimbali za kupelekea matokeo mabaya katika ligi Bw. Aveva amesema kwamba utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wachezaji, utendaji usio makini kwa TFF hasa katika swala la upangaji waa ratiba, ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi pia kueleza kwamba waamuzi nao wamechangia kuharibu matokeo ya mchezo mzima

Aidha akiendelea kutaja sababu za kupelekea matokeo mabaya msimu huu Aveva ametaja vyombo vya habari navyo vimekua mstari wa mbele katika kuichanganya klabu ya Simba kwa kupotosha habari na kwamba tayari wameshaanza kuchukua hatua kwa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimetoa ripoti ambazi siyo za kweli

Hata hivyo Bw. Aveva amesema kwamba kwa sasa uongozi unaangalia jinsi ya kuboresha timu kwa kusajili wachezaji wenye viwango na watakaoendana na timu ya Simba, na na pia kuboresha benchi la ufundi ambalo lilionekana kuwa na changamoto katika msimu huu

Pamoja na hayo Rais huyo wa klabu ya Simba amejibu tuhuma za kutokuwalipa wachezaji mishahara kwa wakati na kudai kuwa mishahara asilimia kubwa inatoka kwa wadhamini hivyo suala la kuchelewa kidogo ni jambo la kawaida kwani hata wachezaji wake wanaelewa tarehe maalumu za kuchukua fedha na kuongeza kama siku zilizdi ni jambo la dharura.

Sanjari na hayo Bw. Aveva ameto rai kwa wanachama hai wa klabu ya Simba kujitokeza kwa wingi katika Mkutano mkuu utakaofanyika Julai 10 ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kushauriana jinsi ya kuendesha na kutatua baadhi ya matatizo yanayoikabili klabu hiyo.

Magufuli atishia kuwatumbua jipu mawaziri wawili walioanza na JK
Kafulila apigwa chini rasmi, Mahakama yamhalalisha Mwilima