Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Avram Grant ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 26 ambacho kitapunguzwa na kubaki na wachezaji 23 tayari kwa fainali za Afrika za mwaka 2015 ambazo zitaanza kuunguruma Januari 14 nchini Gabon.

Katika kikosi hicho Grant aliyewahi kuwa meneja wa muda wa klabu ya Chelsea ya England, amewajumuisha kwa mara ya kwanza wachezaji Ebenezer Ofori, Joseph Larweh Attamah, Bernard Tekpetey na Rahpael Dwamena huku akiwatema Kwadwo Asamoah wa Juventus na Jeffery Schlupp wa Leicester City.

Viungo Kevin-Prince Boateng na Sulley Muntari wameendelea kukosekana kikosini licha ya mara kadhaa kuomba kurejeshwa.

Ikumbukwe mwaka 2014 katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil, Boateng na Muntari waliondoshwa kikosini kwa utovu wa nidhamu.

Asamoah Gyan, Mubarak Wakaso, Christian Atsu na ndugu wawili wa damu Andre Ayew na Jordan Ayew wamepewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji ya Ghana.

Ghana itaweka kambi ya siku chake huko falme za kiarabu kabla ya Januari 4, ambapo kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitatangazwa na kocha Grant.

Ghana impengwa katika kundi D pamoja na Mali, Misri na Uganda na itaanza kupeperusha bendera yake Januari 17 pale itakaposhuka dimbani kuvaana na Uganda.

Kikosi Kamili.

Makipa: Razak Braimah (Cordoba,Spain), Adam Kwarasey (Rosenborg,Norway) Richard Ofori (Wa All Stars)

Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, USA),  Andy Yiadom (Barnsley, England), Baba Rahman (Schalke, Germany), Frank Acheampong (Anderlecht, Belgium), (John Boye (Sivasspor, Turkey), Jonathan Mensah (Anzhi, Russia), Daniel Amartey (Leicester City, England) na Edwin Gyimah (Orlando Pirates, South Africa)

Viungo: Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italy), Afriyie Acquah (Torino, Italy), Thomas Partey (Atletico Madrid, Spain) Mubarak Wakaso (Panathinaikos, Greece), Christian Atsu (Newcastle, England), Ebenezer Ofori (AIK Stockholm, Sweden), Samuel Tetteh (Leifering, Austria) na Joseph Larweh Attamah (BaÅŸakÅŸehir,Turkey)

Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ahli, UAE) Jordan Ayew (Aston Villa, England), Abdul-Majeed Waris (Lorient, France), Andre Ayew (West Ham, England), Ebenezer Assifuah (Sion,Switzerland), Bernard Tekpetey (Schalke, Germany), Rahpael Dwamena (Austria Lustenau, Austria)

 

Wema Sepetu, Rapper Future wauanza mwaka kwa style moja
Take one kurudi tena hewani