Mwasiti Hassani (21) anatuhumiwa kwa kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala mtoto mchanga wa wiki mbili Frank Raiton na kutoweka naye Machi 18 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alionekana eneo la tukio nyakati za mchana katika eneo la utulivu Mwabepande manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam.

Akizungumza na gazeti la majira baba wa mtoto Raiton Rudovika amesema mtuhumiwa aliamua kufanya tukio hilo wakati ambapo mama wa mtoto akiwa anaendelea na kazi za ndani.

”ilikuwa majira ya saa moja jioni ndipo ulipotokea mkasa wa binti huyo kuvunja ukuta wa chumba changu na kuondoka na mtoto wakati  mama watoto alikuwa katika majukumu yake ya nyumbani” amesema Raiton

Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwa, mtaani hapo alifika binti mmoja ambaye alikuwa akihitaji kiwanja cha kununua na alikuwa akiishi kwa wakwe zake akisubiri siku zake za kujifungua,.

Baada ya kufika kwa wakwe wa binti huyo na kuwaeleza tukio zima  Baba mkwe wake alionyesha ushirikiano, na kuwapeleka kwa shangazi yake ambako ndiko alipojifungulia.

Hata hivyo baada ya mahojiano ya muda mfupi ukweli ulibainika na kuamuriwa mtu na shangazi yake kupelekwa kituo cha polisi Magwepande ambapo taarifa za tukio zilikua zimekwisha fika.

Kutokana na kukaa muda mrefu bila ya mtoto kupata joto la mama iliamuriwa mtoto kupelekwa kituo cha afya kwaajili ya uangalizi wa madaktari hivyo alipelekwa katika hispitali ya Mwananyamala na kukutwa na ugonjwa wa nimonia.

Naye mwenyekiti wa shina namba 18 James Tarimo amesema kuwa taarifa za kupatikana kwa mtoto aliyekuwa ameibiwa na kusisitiza kuwa sheria zichukue nafasi yake ili kukomesha matendo ya aina hii.

Afrika Kusini: Yawekwa karantini siku 21
Zanzibar: Wananchi 65 wawekwa karantini wakiwemo vigogo wa serikali

Comments

comments