Mwananchi mmoja nchini Afrika Kusini amejikuta akiwekwa kwenye Jeneza huku akiwa hai na wakulima wawili wa Kizungu mara baada ya kukatisha shambani mwao bila idhini yao.

Aidha, Victor Mlotshwa alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika safari zake, ambapo mara baada kukatiza shambani humo wakulima hao walimkamata na kumweka ndani ya jeneza huku wakitishia kumwagia Petroli na kumchoma moto.

Wakulima hao wamefikishwa mahakamani kwaajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili huku kesi hiyo ikivuta hisia za watu wengi nchini humo kufuatia tukio hilo ambalo linaashiria ubaguzi wa rangi.

Hata hivyo, washtakiwa hao Willem Oothuizen na Theo Jackson walikamatwa mwezi novemba mwaka jana baada ya video ya tukio hilo kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii.

Ifahamu saikolojia ya ubongo
Uingereza kuanza majaribio ya manowari yake ya Kijeshi baharini