Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kumkamata mhandisi wa maji wilayani humo, Boniface Lukoho na kuagiza kutafutwa kwa mkandarasi M/S SAGUCK ENGINEERING baada ya kukagua mradi wa maji Katoke ulioanza kujengwa novemba 2013 na kutakiwa kukamilika mei 2014, wenye thamani ya shilingi milioni 467 na zaidi ya shilingi milioni 400 zikiwa zimeshalipwa huku mradi huo ukiwa bado haujakamilika.
 
Amefikia umuzi huo mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa maji na kubaini kuwa mradi huo hautoi maji licha ya mkandarasi huyo kulipwa hela kwa asilimia 90, ambapo kwa nyakati tofauti tofauti wananchi hao wamemwambia naibu waziri kuwa tangu mradi huo uanze kujengwa katika kata yao hawakuwahi kushirikishwa.
 
“Haiwezekani serikali tutoe fedha kubwa kiasi hicho mradi ukamilike mhandisi uupokee na kuridhika nao wananchi wasipate maji, mkandarasi amenitumia ujumbe hapa kuwa mabomba ya maji mlikuwa mkinunua nyie mnampatia yeye alaze na mambomba hayo yote yamepasuka na hapa kanitumia video mabomba yakimwaga maji, nipo tayari kupoteza kazi lakini wananchi wapate haki yao na kwa kuwa mmeshindwa kuchukua hatua mimi ngoja nichukue hatua,” amesema Aweso.
 
Aidha, kufuatia manung’uniko hayo kutoka kwa wananchi naibu waziri akamuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Muleba kumkamata mhandisi wa maji huku akiwataka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba {BUWASA} kutokana na ufanisi mkubwa walionao katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji mkoani Kagera kuanza kuushughulikia mradi huo kwa haraka ili wananchi waanze kupata maji.
  • Mafao yamponza mstaafu auawa na ‘House boy’
  • Video: Zitto ‘aiteka’ Chadema, Mbowe anyang’anywa ofisi ya ubunge
  • Kamanda wa Polisi afunguka askari watatu kumpa kibano dereva
 
Katika hatua nyingine naibu waziri akiwa wilayani Biharamlo amemsimamisha kazi mhandisi wa maji wilayani humo PATRICE JEROME kwa udanganyifu hii imetokana na naibu waziri kusimamisha msafara wake alipokuwa akitokea wilayani Ngara na kuwakuta wananchi katika mji mdogo wa Nyakahula waliokuwa wamebeba madumu wakilia na kero ya ukosefu wa maji huku kukiwa na mradi mkubwa wenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 na haufanyi kazi.
 
Hata hivyo, mara baada ya kuwasikiliza wananchi wakaamua kumtembeza katika dp za maji na kujionea hali halisi ya kuwa maji hayatoki na kuamua kufanya uamuzi wa kumsimamisha kazi mhandisi wa maji wa wilaya hiyo

SADC yaikaba koo CENI, yataka kura zirudiwe kuhesabiwa Congo DR
Mafao yamponza mstaafu auawa na 'House boy'